IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Waandamanaji wazuia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Uholanzi

19:02 - January 14, 2024
Habari ID: 3478195
IQNA - Polisi wameshambulia waandamanaji waliokuwa wanapinga mpango wa kuteketeza moto nakala ya Qur’ani Tukufu, mpango ambao ulikuwau umepangwa na mkuu wa vuguvugu la kupinga Uislamu la PEGIDA, Edwin Wagensveld, katika mji wa Arnhem nchini Uholanzi.

olisi walisema wametoa kibali kwa kikundi cha mrengo wa kulia cha PEGIDA kuchoma nakala ya Qur’ani Tukufu, lakini kundi la waandamanaji waliwazui siku ya Jumamosi.

Waandamanaji watatu walikamatwa kwa kile kilichoelezwa kutotii polisi na maafisa watatu walijeruhiwa katika purukushani hizo.

Wagensveld aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya tukio hilo.

Meya wa Arnhem, Ahmed Marcouch, ambaye ana asili ya Morocco, alisema kuwa kuchoma kitabu kitakatifu sio kinyume cha sheria nchini Uholanzi.

Hata hivyo, alikiri kuwa kitendo hicho kilikuwa cha uchochezi na kinaumiza hisia za watu wengi.

Huko Uholanzi, mameya wana uwezo wa kupiga marufuku maandamano ikiwa yatahatarisha utulivu wa umma.

Yildirim Usta, mjumbe wa baraza kutoka Chama cha Denk huko Arnhem, alimlaani Marcouch kwa kutoa kibali cha kuchoma nakala ya Qur’ani Tukufu kwa vuguvugu la PEGIDA

Alisema PEGIDA inahusika na uhalifu wa chuki kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Pia alielezea kutoridhishwa na jinsi polisi wanavyowatendea waandamanaji Waislamu na kusema kuwa atapendekeza hatua kali zaidi dhidi ya uhalifu wa chuki katika baraza la manispaa.

Wagensveld amehusika katika matukio kadhaa ya uchomaji wa nakala  za Qur’ani Tukufu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mnamo 2022 na 2023, aliripotiwa kuchoma au kurarua nakala ya Qur’ani Tukufu mbele ya jengo la muda la bunge la Uholanzi huko The Hague na katika maandamano ya peke yake huko Utrecht.

Pia alikamatwa huko Rotterdam na The Hague kwa kujaribu kuchoma nakala ya Qur’ani Tukufu bila kufuata sheria za maandamano.

Katika matukio yote mawili, vikundi vya Waislamu vilifanya maandamano kupinga vitendo vya PEGIDA.

Mwaka jana, Wagensveld pia alirarua nakala ya Qur’ani Tukufu mbele ya Ubalozi wa Uturuki huko The Hague.

Habari zinazohusiana
captcha