Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa suala muhimu kwa harakati hiyo ni kwamba inaungwa mkono na wananchi wa Lebanon, mataifa ya Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu.
2013 Jul 25 , 14:42
Spika wa Majlisi ya Kiislamu ya Iran (bunge) Ali Larijani amelaani vikali hatua ya Umoja wa Ulaya kuliwekea vikwazo tawi la kijeshi la harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kusema nchi hizo 28 za Ulaya zinafuata kibubusa na kupokea maagizo kutoka Marekani.
2013 Jul 25 , 14:41
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Wamarekani hawaaminiki, wasiotumia mantiki na sio wakweli wa kufanya nao miamala.
2013 Jul 22 , 22:31
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewaandalia Waislamu futari katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi ambapo amesisitiza kuwa serikali yake inataka kuwaunganisha Wakenya wote.
2013 Jul 21 , 13:52
Abbas Araqchi msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la kigaidi lililofanywa katika haram tukufu ya Bi Zainab (AS) huko katika viunga vya Damascus mji mkuu wa Syria.
2013 Jul 20 , 16:57
Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vijavyo kwanza unapaswa kufikia hatima ya miji ya utawala huo ghasibu kabla ya kuishambulia Bairut, na kusisitiza kwamba Israel haina ubavu tena wa kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon.
2013 Jul 20 , 16:56
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran Ayatullah Ahmad Janati, amesema kuwa, hali ya mambo ya nchini Misri na kuendelea mapigano na mauaji nchini humo, ni mambo yanyotia wasiwasi mkubwa.
2013 Jul 20 , 16:56
Katika siku ya tano ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, amekutana na Rais Mahmoud Ahmadinejad pamoja na baraza lake la mawaziri, na kusifu kazi na juhudi zake kubwa za usiku na mchana katika kuhudumia taifa na kudumisha kaulimbiu ya mapinduzi katika nyuga mbalimbali, ndani na nje ya nchi.
2013 Jul 15 , 15:34
Rais-mteule wa Iran Hassan Rohani amesema Tehran inapinga vikali vita na mizozano baina ya Waislamu na kwamba itajaribu kila liwezekanalo kuzuia hali kama hiyo.
2013 Jul 14 , 11:25
Mwendesha Mashtaka nchini Misri ameamuru kutiwa mbaroni viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Ikwanul Muslimin akiwemo kiongozi mkuu wa harakati hiyo Mohammad Badie.
2013 Jul 11 , 15:48
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezungumzia hali ya sasa ya Misri na kitendo cha jeshi la nchi hiyo cha kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Mursi na kusema, Misri ni kituo cha mwamko wa Kiislamu na kwamba wale waliopewa dhima ya kuunda serikali baada ya mapinduzi ya wananchi Waislamu walijitayarishia uwanja wa kupinduliwa na kuondolewa madarakani.
2013 Jul 06 , 17:01
Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamefunguliwa leo mjini Tehran na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2013 Jul 06 , 16:59
Rais-mteule wa Iran Sheikh Hassan Rohani amesema kuwa msimamo wa wastani na busara ni mambo ambayo yataiwezesha Iran kukabiliana na matatizo ya kitaifa, kieneo na kimataifa.
2013 Jul 04 , 16:40