Rais-mteule wa Iran Sheikh Hassan Rohani amesema kuwa msimamo wa wastani na busara ni mambo ambayo yataiwezesha Iran kukabiliana na matatizo ya kitaifa, kieneo na kimataifa.
2013 Jul 04 , 16:40
Banki moja ya Kiislamu Kenya ijulikanayo kama Gulf African Bank imesema itafungua tawi lake nchini Tanzania baadaye mwaka 2014 kwa lengo la kuwahudumia Waislamu nchini humo.
2013 Jun 30 , 13:55
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema nchi chache zinazojitakia makuu zinazuia utatuzi wa kadhia ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2013 Jun 27 , 18:14
Mauaji ya kutisha yaliyofanywa dhidi ya Waislamu wa Kishia katika kijiji cha Zawiyat Abu Muslim mkoani Giza nchini Misri yanaendelea kulaaniwa ndani na nje ya nchi hiyo.
2013 Jun 25 , 12:29
Shirika la Ndege la Kenya Airways limeongeza maradufu safari zake zake katika mji wa Jeddah, Saudi Arabia kabla ya kuanza msimu wa Hijja mwaka huu.
2013 Jun 25 , 12:25
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amewataka maulama katika ulimwengu wa Kiislamu kujiepusha na matamshi yoyote ambayo yatapelekea kutokea fitina na mifarakano.
2013 Jun 23 , 11:06
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Abbas Araqchi amesema Tehran inapinga mazungumzo ya Markekani na wanamgambo wa Taliban huko Doha, mji mkuu wa Qatar.
2013 Jun 23 , 10:57
Khatibu wa sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema kuwa duru ya 11 ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ushindi adhimu kwa taifa la Iran katika chimbuko la hamasa ya kisiasa.
2013 Jun 21 , 21:48
Hivi karibuni mwanamke Mwislamu aliyekuwa amevaa Hijabu alishambuliwa na magenge ya kibaguzi ya Wanazi mamboleo katika kitongoji cha Paris cha Argenteuil.
2013 Jun 21 , 12:47
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo asubuhi ameongoza mamilioni ya Wairani katika zoezi la upigaji kura ambapo amepiga kura yake na kuwataka wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.
2013 Jun 14 , 21:58
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema kuwa, kufanyika uchaguzi uliofana kwa kushiriki wananchi wengi, kunainua uwezo na maendeleo makubwa ya mfumo wa Kiislamu ndani ya Iran na katika nyuga mbalimbali za kimataifa.
2013 Jun 14 , 21:56
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na wahadhiri, maqarii na mahafidh wa Qur’ani Tukufu walioshiriki kwenye Mashindano ya Thelathini ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya mjini Tehran na kutaja moja ya mafundisho makubwa ya Qur’ani Tukufu ni kuwataka Waislamu walinde umoja, mshikamano, mapenzi na ushirikiano baina yao.
2013 Jun 08 , 22:19
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametahadharisha kwamba adui anafanya njama za kuzusha mfarakano baina ya mataifa ya Kiislamu ili kuzuia umma wa Kiislamu usisonge mbele.
2013 Jun 08 , 11:01