Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran kwenye duru ya 11 ya uchaguzi wa rais hapa nchini, kutaulinda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na njama za maadui.
2013 May 24 , 20:59
Jeshi la Nigeria linaendeleva vita dhidi ya kundi haramu la Mawahabbi lijulikanalo kama Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema waasi wa Boko Haram wamedhoofika na kwamba wanaikimbia nchi hiyo kwa idadi kubwa baada ya kushambuliwa.
2013 May 21 , 21:23
Maandamano ya kulalamikia hatua ya askari wa usalama wa Bahrain ya kuvamia nyumba ya Sheikh Issa Ahmed bin Qassim mwanazuoni maarufu wa nchi hiyo, bado yanaendelea.
2013 May 21 , 21:22
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, 'katika kufikia malengo yao na kuvunja njama za maadui, wananchi wa Iran watajitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao wa rais na kumchagua mgombea aliye bora ili aweze kuchukua jukumu zito la kusimamia ustawi na ezza ya taifa.'
2013 May 16 , 14:49
Jana Jumatano tarehe 15 Mei, ilikuwa siku ya kukumbuka kutimia miaka 65 tangu ardhi za Palestina zilipokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, siku inayojulikana kama 'Siku ya Naqba.'
2013 May 16 , 14:48
Siku mbili baada ya Mawahabi kuharibu kaburi la Sahaba wa Mtume (saw) Hujr bin Adi nchini Syria, wafusi wa kundi hilo nchini Jordan wamefanya maafa mengine na kuchoma moto Haram ya Swahaba Jafar bin Abi Twalib maarufu kwa jina la Jafar Tayyar, radhi za Mwenyenzi Mungu ziwe juu yake, huko kusini mwa nchi hiyo.
2013 May 05 , 09:50
Mawahabi na magaidi wa Syria wamevunja kaburi la Sahaba maarufu wa Mtume Muhammad (saw) Hujr ibn Adi Al Kindi nchini Syria na kufukua mwili wa Sahaba huyo aliyeuwa shahidi kwa amri ya Muawiya bin Sufiyan.
2013 May 05 , 09:50
Mkutano wa Kimataifa wa Maulamaa na Mwamko wa Kiislamu umeanza Jumatatu Aprili 29 mjini Tehran ukihudhuriwa na mamia ya wasomi, wanafikra na wanazuoni wa kidini kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu. Mkutano huo umefunguliwa kwa hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Ayatullah Ali Khamenei.
2013 Apr 30 , 21:20
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei Jumamosi hii (27 Aprili) amehutubia hadhara kubwa ya maelfu ya wafanyakazi, wadau wa sekta ya uzalishaji na wafanyakazi bora. Ameashiria haja ya nchi kwa hamasa na harakati kubwa katika medani za uchumi na siasa na kuutaja uchaguzi kuwa ni muhimu na medani ya kudhihiri uwezo na nguvu ya taifa.
2013 Apr 28 , 21:13
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki ametoa wito kwa Waislamu Iraq kudumisha umoja na kusema machafuko ya kimadhehebu nchini humo yameibuliwa na watu wanaopata himaya kutoka nchi za kigeni.
2013 Apr 28 , 21:12
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Sheikh Kadhim Siddiqi amesisitizia juu ya mwamko na mshikamano wa Waislamu kwa ajili ya kukabiliana na njama za maadui na vitisho vya mabeberu dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.
2013 Apr 26 , 21:52
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa kongamano la kimataifa la ‘Maulamaa na Mwamko wa Kiislamu’ ambalo litafanyika Tehran wiki ijayo.
2013 Apr 26 , 21:51
Vikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kufanyika mashindano ya magari ya langa-langa ya Formula One Grand Prix ambayo yanatazamiwa kuanza leo katika mji mkuu, Manama.
2013 Apr 21 , 13:43