Vikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kufanyika mashindano ya magari ya langa-langa ya Formula One Grand Prix ambayo yanatazamiwa kuanza leo katika mji mkuu, Manama.
2013 Apr 21 , 13:43
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani ina mtazamo unaokinzana kuhusu mauaji ya watu wasio na hatia.
2013 Apr 18 , 14:06
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, uchaguzi ujao wa rais nchini Iran utafanyika kwa hamasa na mahudhurio makubwa na kuwashangaza tena walimwengu.
2013 Apr 13 , 19:13
Msikiti mmoja katika kitongoji cha mji mkuu wa Sweden, Stockholm umeruhusiwa kuadhini kwa kutumia kipaza sauti kilicho kwenye mnara kwa ajili ya Sala ya Ijumaa. Hii ni mara kwa kwanza kwa nchi hiyo ya Scandinavia kuruhusu adhana kwa sauti inayosikika nje ya msikiti.
2013 Apr 13 , 19:13
Kiongozi Muadhamu katika mazungumzo yake na Rais wa Burundi:
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khameni mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliyeko safarini hapa nchini. Ayatullah Khamenei ameashiria mtazamo chanya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nchi za Kiafrika na kusisitiza kuwa, Iran inakaribisha ustawi na maendeleo ya nchi za Kiafrika na umoja miongoni mwao.
2013 Apr 10 , 21:18
Shirika la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA) limetangaza mpango wa kujenga misikiti 1110 mipya katika maeneo mbali mbali kote Iran.
2013 Apr 07 , 11:17
Wanafunzi kadhaa wataiwakilisha Uganda katika Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Kuwait.
2013 Apr 07 , 11:06
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema kuwa, njama za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zenye lengo la kuwavunja moyo wananchi wa taifa hili kutokana na kujichagulia mfumo wa Kiislamu kuwaongoza, zimegonga mwamba.
2013 Apr 06 , 19:32
Jamii ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Pakistan imefanya maandamano makubwa katika mji wa Karachi ikilaani serikali ya Myanmar kwa kushirki katika mauaji ya Waislamu wa nchi hiyo.
2013 Apr 06 , 17:40
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameashiria matamshi yanayotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushambulia taasisi za nyuklia za Iran na kusema kuwa, Israel inajua na kama haijui inapaswa kutambua kwamba, iwapo itajaribu kufanya hivyo makombora ya Iran yataisawazisha na udongo miji ya Tel Aviv na Haifa.
2013 Mar 23 , 11:49
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ujumbe wa Nowruz kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1392 Hijria Shamsiya na kusisitiza kuwa taifa la Iran litaendelea na harakati ya kuvunja kikamilifu njama za maadui. Ameongeza kuwa taifa la Iran liteendelea na njia yake ya ustawi katika nyanja zote ili kufikia uadilifu wa kimataifa.
2013 Mar 20 , 22:19
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutangaza mwaka mpya wa 1392 Hijria Shamsiya kuwa, 'Mwaka wa Hamasa ya Kisiasa na Hamasa ya Kiuchumi' kwa taifa la Iran.Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei katika ujumbe wa Nowruz alioutoa kwa mnasaba wa kuanza mwaka 1392 Jumatano ya leo.
2013 Mar 20 , 22:15
Binti mmoja wa Kifaransa aliyevalia vazi la stara la hijabu, amezuiliwa kujiandikisha kwenye somo la michezo kwa sababu eti amevaa vazi hilo la stara kwa mwanamke wa Kiislamu.
2013 Mar 20 , 19:02