Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema historia ya Mapinduzi ya Kiislamu, Kujihami Kutakatifu, Palestina na Mwamko wa Kiislamu ni kati ya maudhui ambazo ni muhimu zitumike katika utengenezaji filamu.
2013 Feb 21 , 16:00
Kamanda wa vikosi vya nchi kavu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi zinatoa fedha na kuunga mkono operesheni za kigaidi ndani ya Iran.
2013 Feb 21 , 16:00
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi makubwa yaliyofanywa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika soko moja karibu na mji wa Quetta huko kaskazini magharibi mwa Pakistan.
2013 Feb 18 , 15:56
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano ya kila mwaka ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni mithili ya dharba nzito inayowashukia maadui na wapinzani wa taifa la Iran na kusisitiza kwamba mwaka huu pia hivyo ndivyo ilivyokuwa.
2013 Feb 17 , 20:48
Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amesema harakati ya mapambano au muqawama Lebanon iko tayari kuilinda nchi hiyo endapo utawala haramu wa Israel utathubutu kutekeleza hujuma dhidi yake.
2013 Feb 17 , 20:47
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, maadui wametambua kwamba hawawezi kukabiliana na taifa la Iran.
2013 Feb 11 , 21:03
Mamilioni ya wananchi wa Iran ya Kiislamu wameshiriki kwa hamasa na shauku kubwa katika maadhimisho ya miaka 34 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadhimisho ambayo yalifikia kileleni jana Jumapili.
2013 Feb 11 , 14:18
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo ameshiriki kwenye maandamano ya tarehe 22 Bahman yaani siku zinapofikia kileleni sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika uwanja wa Azadi yaani Uhuru, hapa mjini Tehran yaliyohudhuriwa pia na umati mkubwa wa wananchi, viongozi mbalimbali wa serikali na wanazuoni wa kidini, na kupongeza kuwadia mwaka wa 34 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
2013 Feb 10 , 22:26
Ayatullah Muhammad Ali Mowahedi Kermani Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ulioongozwa na Imam Khomeini MA, ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo imewapa wananchi wa Iran izza na utukufu na kuwaepusha na vitendo vya dhulma, ukandamizaji na ukoloni.
2013 Feb 08 , 19:26
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema viongozi wa Marekani hawana nia njema katika matamshi yao ya kutaka mazungumzo na Iran.
2013 Feb 08 , 19:26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema nchi za Magharibi zimeanzisha kampeni mpya ya kulitawala bara la Afrika na kwamba hilo limetokana na hitilafu baina ya Waislamu na kujishughulisha na migongano baina yao.
2013 Jan 29 , 22:11
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka Waislamu wa madhehebu na mataifa yote duniani kuungana juu ya misingi na malengo makuu ya Uislamu na kusisitiza kwamba kupambana hadi kuuangamiza Uzayuni inabidi liwe ni moja ya malengo hayo makuu ya Waislamu.
2013 Jan 27 , 21:32
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, imepangwa mikakati maalumu ya kumvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW na dini tukufu ya Kiislamu na jambo hilo linatoa changamoto kubwa kwa umma wa Kiislamu.
2013 Jan 26 , 11:46