Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, imepangwa mikakati maalumu ya kumvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW na dini tukufu ya Kiislamu na jambo hilo linatoa changamoto kubwa kwa umma wa Kiislamu.
2013 Jan 26 , 11:46
Ayatullah Kashani, Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, umoja wa Waislamu ndio utakaokuwa chimbuko la ushindi wao dhidi ya njama mbalimbali za uistikbari na maadui.
2013 Jan 25 , 22:12
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mahmoud Ahmadinejad amewataka Waislamu kote duniani kuungana na kuzima njama za maadui.
2013 Jan 24 , 22:29
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge amezitaka nchi za Kiislamu kufanya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano kati ya mataifa ya Kiislamu katika hali nyeti ya hivi sasa.
2013 Jan 23 , 13:17
Iran inatazamia kuwa mwenyeji wa kongamano la 26 la kimataifa la Umoja wa Kiislamu litakalohudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 102 duniani.
2013 Jan 20 , 20:18
Jumuiya ya Waislamu Mashia Tanzania (TIC) imefanya mkutano hivi karibuni katika mji mkuu wa Tanzania Dar es Salaam kwa lengo la kutambuana, kujuana na kufahamiana. Katika mkutano huo Waislamu wametakiwa kujitegemea kiuchumi.
2013 Jan 20 , 20:18
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafungua kambi maalumu nchini Myanmar kwa lengo la kuwasaidia Waislamu wanaodhulumiwa nchini humo.
2013 Jan 20 , 20:18
Pote la Uwahabi ndio tishio la pili kwa ukubwa katika Ummah wa Kiislamu baada ya Marekani na utawala wa Kizayuni amesema khatibu maarufu wa Sala ya Jumaa nchini Tunisia Sheikh Abdul Latif Musa.
2013 Jan 19 , 17:16
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amelaani mauaji ya kigaidi ya Waislamu wa Pakistan, Iraq na Syria na kusema kwamba magaidi wanafanya jinai na kutekeleza malengo ya Marekani katika eneo kutokana na msaada wa fedha na kijeshi wa Washington.
2013 Jan 19 , 17:16
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuendelea kuwepo Mapinduzi ya Kiislamu, uwezo na ustawi wa Iran licha ya mashinikizo ya maadui katika kambi ya istikbari ya kimataifa ni shara ya kutimia kivitendo ahadi ya Allah SWT.
2013 Jan 17 , 14:00
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la The Times la utawala haramu wa Israel unaonyesha kuwa idadi kubwa ya Wazayuni hawatilii maanani porojo za kila siku za Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba Iran inakaribia kumiliki silaha za nyuklia.
2013 Jan 15 , 14:33
Makumi ya maelfu ya watu wa Pakistan wameandamana kupinga mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.
2013 Jan 14 , 11:35
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, vijana azizi wa taifa la Iran wanapaswa kujiweka tayari kwa ajili ya kupiga hatua zenye kasi kubwa za maendeleo kuelekea kwenye malengo matukufu yaliyoainishwa.
2013 Jan 14 , 11:35