Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema kuwa, katika kipindi cha miaka 33 iliyopita, taifa la Iran limeweza kushinda njama zote za Wamagharibi za kuizuia Jamhuri ya Kiislamu isifikie hatua ya kujitosheleza katika nyanja mbalimbali.
2012 Nov 04 , 11:50
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ikiwa mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati na mengineyo yatathubutu kutenga siku moja na kuitangaza kuwa ni siku ya kujibari na Marekani, basi bila ya shaka yoyote mataifa hayo yatakuwa yamepiga hatua kubwa ya kihistoria.
2012 Nov 01 , 17:31
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amesema jeshi la nchi hii lina uwezo wa kiulinzi ambao umeiwezesha Jamhuri ya Kiislamu kudumusha uthabiti na usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
2012 Oct 28 , 11:59
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka serikali ya Myanmar kulinda haki za kimsingi za Waislamu nchini humo.
2012 Oct 28 , 11:58
Maelfu ya wahujaji wa Kiirani na wasio Wairani wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu jana tarehe 9 Dhilhaji walishiriki katika amali ya kujitenga na kujiweka mbali na washishirikina iliyofanyika katika uwanja wa Arafa.
2012 Oct 26 , 23:44
Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina amesema kuwa utawala wa Israel unazidi kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina na ameitaka jamii ya kimataifa isusie na kuyawekea vikwazo makampuni yanayojishughulisha na ujenzi katika maeneo hayo.
2012 Oct 26 , 23:43
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei ametuma ujumbe kwa mahujaji katika mwaka huu wa 1433 Hijria Qamaria na kusema msimu wa Hija ni fursa ya kutaamali na kuyaangalia kwa kina masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu. Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo.
2012 Oct 25 , 13:20
Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, al Kaaba leo wameelekea Mina kwa ajili ya kutekeleza marasimu na ibada ya siku ya Tarwiya hiyo kesho tarehe 8 Dhilhaji katika eneo hilo tukufu.
2012 Oct 23 , 21:42
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, hatua ya utawala wa haramu wa Israel ya kushambulia meli ya Kiswedeni iliyokuwa imebeba misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya wananchi wa Gaza huko Palestina ni ushahidi wa wazi wa uharamia wa baharani.
2012 Oct 23 , 11:06
Waislamu nchini Myanmar wanaendelea kukabiliwa na mateso na masaibu makubwa kutoka kwa makundi ya Kibudha yenye siasa kali.
2012 Oct 23 , 11:06
Mahakama ya Federali ya Marekani imekataa tena ombi mcheza filamu iliyomvunjia heshima Mtume (saw) aliyeitaka YouTube kuondoa sehemu aliyocheza yeye katika filamu ya Innocence of Muslims.
2012 Oct 20 , 19:55
Serikali ya Saudi Arabia imesema Waislamu wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu kutokana na kuibuka ugonjwa wa Ebola katika nchi hizo mbili za Afrika.
2012 Oct 20 , 19:55
Khatibu wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema, ulimwengu wa kibeberu unapaswa kutambua kwamba, taifa la Iran limestahamili magumu mengi na kwamba, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu litashinda njama na mipango yote ya maadui.
2012 Oct 19 , 22:38