Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unaonesha kuwa idadi ya Wakristo wa Kiprotestanti imepungua na kufikia chini ya asimilia 50 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo.
2012 Oct 10 , 23:04
Mwanamke kutoka Bosnia amekuwa meya wa kwanza nchini Bosnia na barani Ulaya kuvaa vazi la stara la Kiislamu, Hijabu.
2012 Oct 10 , 22:57
Kampuni ya Kimarekani inayotengeneza na kusambaza michezo ya kompyuta ya Activision imepiga marufuku uuzaji wa moja ya michezo yake unaowafutia watu wengi kutokana na kuwa na vipengee vinavyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
2012 Oct 09 , 13:33
Serikali ya Ufilipino imefikia mwafaka na kundi kubwa kabisa nchini humo la wapiganaji wa Kiislamu la Moro Islamic Liberation Front (MLF) ambalo limekuwa likitaka kujitenga eneo la kusini mwa nchi hiyo.
2012 Oct 09 , 13:33
Makumi ya maelfu ya wananchi wameandamana Jumapili usiku katika mji weenye utajiri wa mafuta mashariki mwa Saudi Arabia.
2012 Oct 09 , 06:58
Waisraeli wa utawala ghasibu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamechukizwa mno na hatua ya kampuni ya simu ya Apple ya kutouonesha mji wa baitul Muqaddas (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel katika simu yake mpya aina ya Iphone 5.
2012 Oct 08 , 18:23
Waislamu wa pembe mbalimbali ulimwenguni wameendelea kulaani filamu ya Kimarekani ya "Innocence of Muslims" inayomvunjia heshima Mtume saw.
2012 Oct 08 , 12:29
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetoa taarifa ikilaani vikali jinai za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel dhidi ya matukufu ya Kikristo na Kiislamu katika msikiti mtukufu wa al-Aqsa.
2012 Oct 06 , 21:36
Watawala wa Qatar wamechukua hatua ya kushangaza na isiyo ya kibinadamu ya kupiga marufuku Mashia wa Lebanon kuingia nchini humo.
2012 Oct 06 , 21:30
Mahakama moja nchini Kazakhstan imepiga marufuku filamu ya Marekani inayomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
2012 Oct 06 , 21:27
Viongozi wa Kiislamu, Kiyahudi, Kibuda na Kikristo kaskazini mwa Ufaransa wamelaani vikali vitendo vya kuendelea kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.
2012 Oct 06 , 21:25
Jaji mmoja wa mahakama ya serikali kuu ya Marekani mjini Washington DC jana Ijumaa alikiruhusu kikundi kimoja cha Wazayuni kilicho na misimamo ya kupindukia mipaka kuweka mabango yaliyo na matangazo ya chuki dhidi ya Uislamu katika vituo vya treni ya chini kwa chini mjini humo.
2012 Oct 06 , 21:17
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesisitiza kuwa sababu kuu ya mashinikizo yote yanayotolewa dhidi ya Iran ni msimamo huru wa taifa la Iran na kutosalimu amri mbele ya mfumo wa kibeberu duniani.
2012 Oct 03 , 22:10