Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza maazimio yanayopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
2012 Oct 01 , 18:44
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya Iraq na kuua makumi ya watu wasiokuwa na hatia.
2012 Oct 01 , 18:16
Uamuzi wa Marekani wa kuliondoa kundi la kigaidi la Munafiqina yaani MKO kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi umeandamwa na radiamali mbalimbali.
2012 Oct 01 , 15:52
Zaidi ya Wairani 75000 watashiriki katika ibada ya Hija mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, safari za ndege za Hija zimeanza Septemba 24 na kila siku mahujaji 3000 watasafirishwa kuelekea Madina na Jeddah.
2012 Oct 01 , 15:50
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kwamba, madai ya Bahrain kwamba, Tehran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo hili hayana msingi wowote.
2012 Oct 01 , 15:48
Maelfu ya wakaazi wa mji wa Michigan nchini Marekani wameandamana kulaani filamu ya Marekani pamoja na vijikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw) vilivyochapishwa hivi karibuni huko Ufaransa.
2012 Sep 30 , 16:00
Sheikh Abdul Hubail, mwanazuoni wa Kishia nchini Saudia amelaani vikali mauaji ya vijana watatu wa Kishia katika mji wa al Awamiya nchini humo.
2012 Sep 30 , 15:57
Gazeti la al Watan linalochapishwa nchini Misri limejibu dharau na hujuma ya Wamagharibi dhidi ya Mtume wa Uislamu kwa kuchapisha katuni ya kuvutia inayokosoa mwenendo wa nchi za Magharibi kuhusu ulimwengu wa Kiislamu.
2012 Sep 30 , 15:48
Vikosi vya jeshi la utawala wa kifalme wa Saudi Arabia vimemuua shahidi kijana aliyekuwa na umri wa miaka 16 aliyekuwa akiandamana katika eneo la Awamiyya mashariki mwa nchi hiyo.
2012 Sep 30 , 15:10
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ametaka kupigwa marufuku vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW.
2012 Sep 30 , 15:07
Maandamano makubwa dhidi ya Marekani yangali yanaendelea katika nchi za Kiislamu duniani kwa lengo la kulaani utengenezaji filamu ya Kimarekani inayomkashifu Mtume SAW.
2012 Sep 30 , 15:07
Kitendo cha hivi karibuni cha maadui wa Uislamu cha kumfunjia heshima tena Mtume Muhammad Swallallahu Alayhi Waalihi Wassallam, kimewakasirisha mno Waislamu wote ulimwenguni ambao wameonyesha majibu makali dhidi ya maadui hao. Hii si mara ya kwanza kwa maadui wa Uislamu na Waislamu, kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
2012 Sep 29 , 15:03
Mahakama ya Russia imetangaza kuwa, ni marufuku nchini humo kuonyeshwa filamu iliyotengenezwa Marekani ambayo inamtusi na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
2012 Sep 29 , 14:53