IQNA

Mhadhiri Uturuki afungwa jela kwa kuzuia hijabu

11:11 - November 30, 2014
Habari ID: 2613249
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ege kilichoko katika mji wa Izmir nchini Uturuki amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kumzuia mwanafunzi aliyevaa hijabu ya Kiislamu kuingia darasani.

Taarifa za Mahakama kutoka Istanbul zinaeleza kuwa, Rennan Pekunlu mhadhiri wa astrofizikia jana alianza kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na kosa la kumzuia mwanafunzi wake kuingia darasani, kwa sababu tu amevaa vazi la stara la mwanamke wa Kiislamu.

Wakili Murat Faith Ulku anayemtetea mhadhiri huyo mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa, anakusudia kufungua mashtaka dhidi ya hukumu hiyo kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Uturuki, zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Uturuki ni Waislamu.../mh

2613214

captcha