IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

‘EU inawalenga Waislamu kwa uwazi’: Mahakama Kuu yaruhusu marufuku Hijabu kazini

14:38 - November 29, 2023
Habari ID: 3477961
BRUSSELS (IQNA) - Mahakama kuu ya Umoja wa Ulaya imeamua Jumanne kwamba waajiri wa umma katika nchi wanachama wanaweza kupiga marufuku wafanyakazi kuvaa ishara zozote zinazoonekana za imani ya kidini, ikiwa ni pamoja na vazi la staha katika Uislamu, Hijabu, na hivyo kuashiria pigo kwa uhuru wa dini wa mamilioni ya wanawake Waislamu barani humo.

Kesi hiyo ilifikishwa katika Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya (CJEU) na mwanamke Mwislamu ambaye alifanya kazi ya kupokea wageni katika manispaa ya Ans mashariki mwa Ubelgiji. Aliambiwa na mwajiri wake kwamba hangeweza kuvaa Hijabu kazini, na kwamba alipaswa kutii sera mpya inayowataka wafanyakazi wote wafuate msimamo mkali wa kutoegemea upande wowote kwa kutoonyesha alama zozote za kidini au kiitikadi.

Mwanamke huyo alipinga sera hiyo mahakamani, akisema kwamba inakiuka haki yake ya kufuata dini yake kwa uhuru. Pia alidai kuwa sera hiyo ilikuwa ya kibaguzi, kwani iliathiri kwa kiasi kikubwa wanawake wa Kiislamu wanaovaa Hijabu.

CJEU ilikataa hoja zake na kuamua kuwa sera hiyo ni sahihi kwa kile kinachotajwa kuwa ni 'lengo la kisheria' la kuhakikisha mazingira ya kiutawala yasiyoegemea upande wowote.

Mahakama ilisema kwamba mamlaka za umma katika nchi wanachama zina uhuru wa kuamua jinsi ya kuendeleza sera hiyo ya eti kutoegemea upande wowote kwa utumishi wa umma, na kwamba zinaweza kupiga marufuku au kuruhusu uvaaji wa alama za kidini na wafanyakazi wao.

Uamuzi huo ni kikwazo kwa haki za binadamu za wanawake wa Kiislamu barani Ulaya, ambao wanakabiliwa na ongezeko la uadui na ubaguzi kwa sababu ya utambulisho wao wa kidini.

Hukumu ya mahakama hiyo iliongeza wasiwasi uliokuwepo kuhusu usalama, uhuru na haki za Waislamu barani Ulaya na pia kufichua undumakuwili wa Umoja wa Ulaya kuhusu haki za binadamu, uhuru wa kidini na usawa.

Uamuzi wa mahakama hiyo, hata hivyo, ulitarajiwa na mtu yeyote ambaye amekuwa akitazama hatua kwa hatua ya Ulaya kuingia katika chuki dhidi ya Uislamu kwani hatua zinazoongezeka za kuwatenga na hata kuwaharamisha Waislamu ambazo zimekuwa zikiendelea barani Ulaya kwa miaka mingi.

Chuki dhidi ya Uislamu ilishadidi zaidi  duniani kote baada ya mashambulizi ya 9/11 ambayo yalifuatiwa na  kile kinachoitwa "vita dhidi ya ugaidi." Chuki hiyo hatua kwa hatua ilijipenyeza katika siasa kuu za Ulaya katika miaka ya hivi karibuni. Wanasiasa wa Ulaya kutoka asili tofauti za kisiasa walianza kuwalaumu Waislamu kwa migogoro ya kiuchumi, kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, uhamiaji usio wa kawaida, machafuko ya kijamii na ugaidi wa kimataifa.

3486212

captcha