IQNA

Mkutano vya Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu wafanyika Indonesia

16:07 - May 26, 2016
Habari ID: 3470339
Mkutano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu (ICIM) umefunguliwa Jumatano nchini Indonesia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo umefunguliwa Jumatano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia A.M. Fachir huku mada kuu ikiwa ni kusaidia kukuomboa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

"Tunapaswa kutafuta suluhisho kuhusu masuala ya kibinadamu, kadhia ya Palestina ikiwemo," amesema Fachir katika ufunguzi wa mkutano huo ambapo kaulimbiu yake kuu ni "Vyombo vya Habari vya Kiislamu Vimeungana Kulinda Maslahi ya Uislamu, Hasa Kadhia ya Palestina na Quds."

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia amepongeza Mkutano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu (ICIM) kwa kuweka mbele kadhia ya Palestina ili iweze kuzingatiwa duniani.

Amesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika mapambano ya kupigania ukombozi Palestina, eneo ambalo limekuwa ikikaliwa kwa mabavu na Israel kwa zaidi ya miongo sita sasa.

Mkutano vya Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kiislamu umejumuisha washiriki kutoka nchi kadhaa duiani zikiwemo Indonesia, Australia, Iran, Kuwait, Lebanon, Libya, Ufilipino, Malaysia, Nigeria, Singapore, Sudan, Thailand, Tunisia, Uturuki, na Palestina.

Kongamano hilo ambalo limeanza Jumatano limemalizika Alkhamisi hii katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Mkutano huo wa kimataifa wa vyombo vya habari vya Kiislamu umefadhiliwa na kuandaliwa na serikali ya Indonesia ikiwa ni katiak sera zake za kigeni za kuunga mkono ukombozi wa Palestina.

3500991

captcha