IQNA

Ustamaduni

Sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la Msikiti wa Kwanza katika mji mkuu mpya wa Indonesia

17:33 - January 18, 2024
Habari ID: 3478214
IQNA - Maafisa wa Indonesia wameweka jiwe na msingi na kuzindua ujenzi wa msikiti wa kwanza katika mji mkuu mpya wa nchi hiyo.

Rais Joko Widodo Jumatano aliongoza sherehe za uwekaji jiwe la msingi la msikiti wa kwanza wa kitaifa katika eneo la Nusantara.

Serikali ya Indonesia inahamisha mji mkuu hadi kisiwa cha Borneo kuchukua nafasi ya mji unaodidimia wa Jakarta kwenye kisiwa cha Java, na mradi  huo unatazamiwa kugharibu dola bilioni 32 ambapo umepengwa kukamilika mnamo 2045.

Huku awamu ya kwanza ya ujenzi ikitarajiwa kukamilika mwaka wa 2024, Widodo alizindua ujenzi wa majengo mbalimbali huko Nusantara siku ya Jumatano, ikiwa ni pamoja na msikiti, tawi la kampuni kubwa ya huduma ya posta na studio ya matangazo ya mtandao wa redio ya serikali ya RRI.

Msikiti huo wenye thamani ya dola milioni 62 utajengwa katika jengo ambalo hatimaye litakuwa na maeneo mengine ya ibada, kama vile makanisa ya Kikristo, na mahekalu ya Wabudha, Wahindu na Wachina, Widodo alibainisha.

"Thamani ya ujenzi ni takriban rupiah bilioni 940 (dola milioni 62), kwa kuwa msikiti huu utakuwa mkubwa ... natumai msikiti huu utawakilisha anuwai ya watu wa Indonesia na kutumika kama nafasi ya kuongeza imani na ucha Mungu wetu," alisema wakati wa sherehe ya uwekaji msingi.

"Nataka msikiti huu uwe mfano kwa misikiti mingine duniani, na uonyeshe sifa za kipekee za Indonesia."

Ramani ya msikiti wa kitaifa huko Nusantara imetayarishwa na Nyoman Nuarta kwa ombi la Widodo. Nuarta ni mmoja wa wasanii maarufu wa picha wa Indonesia na muundaji wa sanamu refu zaidi nchini, Garuda Wisnu Kencana, iliyoko Bali.

Mzee wa miaka 72 pia ndiye mbunifu nyuma ya miundo mingine kuu huko Nusantara, pamoja na jumba jipya la serikali.

Widodo alizindua rasmi mradi wa mji mkuu mpya mwaka wa 2019, katika kile ambacho kimeonekana na wengi kama jaribio la kutia muhuri urithi wake kabla ya mwisho wa muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani ambao unakamilika mwaka huu.

Zaidi ya Waindonesia milioni 204 watapiga kura mnamo Februari 14 kuchagua rais mpya wa nchi, makamu wa rais na wabunge.

3486853

 

captcha