IQNA

Petroli ya bure kwa mwenye kusoma Qur'ani Jakarta

19:02 - June 18, 2016
1
Habari ID: 3470395
Shirika la moja la mafuta nchini Indonesia linawapa wenye magari petroli ya bure katika mji mkuu Jakarta kwa sharti la kusoma aya za Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wenye magari na pikipiki wanapowasili kujaza petroli katika vituo vya mafuta vya shirika la kiserikali la Pertamina, wanakumbana na mabango yanayotangaza petrol ya bure kwa sharti la kusoma Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakuu washirika hilo wanasema wanalenga kuwahimiza Waislamu wasome Qur'ani wanapofika kituoni hapo.

Vyumba maalumu vya swala vimewekwa katika vituo vya mafuta vya shirika hilo ambapo kumeshuhudiwa idadi kubwa ya waumini wakijumuika katika mpango huo.

Mkaazi mmoja wa Jakarta, Moetawakkir ,ambaye ni kati ya waliofaidika na mpango huo unaotekelezwa katika vituo vitano vya mafuta mjini Jakarta anasema anatazamia kuhitimisha Qur'ani Tukufu mwishoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Sote tunafahamu kuwa tukifanya amali njema tutapata thawabu na malipo. Kwa kusoma Qur'ani Tukufu kila siku, tunapata yakini ya kuhitimisha Qur'ani mwishoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku tangi la mafuta likiwa limejaa," ameongoza Moetewakkir baada ya kusoma Qur'ani kwa muda wa nusu saa kwa siku ya pili mfululizo.

Washiriki wanatakiwa kujaza fomu kabla ya kuelekea katika chumba cha kusalia ambapo wanasoma sehemu yoyote waitakayo ya Qur'ani Tukufu.

Arif Budiman , msimamizi wa kituo cha petroli cha Haryono anasema: "Tunataka kuwashukuru wale wapendao kusoma Qur'ani Tukufu. Tunawapa lita mbili kwa kila sura ya Qur'ani wanayoisoma."

Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 95 ya watu wote milioni 206 nchini Indonesia.

3460124

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Ibrahim hassan
0
0
MashaAllah
captcha