IQNA

Maafa

Moto umeteketeza Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Jakarta, kuba laporomoka

18:39 - October 21, 2022
Habari ID: 3475962
TEHRAN (IQNA) – Kuba kubwa la Msikiti Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Jakarta nchini Indonesia liliporomoka kufuatia moto mkubwa.

Kuba la msikiti huo liliteketea kwa moto mkubwa Jumatano alasiri na kusababisha uharibifu mkubwa katika msikiti huo.

Kwa mujibu wa mkuu wa msikiti huo, Muhammad Subki, moto huo ulizuka wakati wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi walipokuwa wakitekeleza kazi ya ukarabati.

"Moto ulianza kutokea juu ya kuba na kusambaa katika maeneo mengine, lakini hadi sasa haijabainika kilichosababisha moto huo," alisema Subki.

Aliongeza moto huo ulisambaa kwa haraka sana kutokana na upepo mkali na kuteketeza sehemu kubwa ya msikiti huo.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha kuba hilo likiporomoka na kuibua wingu kubwa la moshi mweusi angani.

3480925

captcha