IQNA

Waislamu Kenya

Rais wa Kenya asimamisha hotuba kwa heshima ya Adhana (+Video)

17:17 - March 07, 2023
Habari ID: 3476671
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Kenya William Ruto alisitisha hotuba yake siku ya Jumatatu ili kuonyesha heshima kwa Adhan, ambayo pia inajulikana kama wito wa Kiislamu kwa maombi.

Ruto, ambaye ni Mkristo, alisimamisha hotuba yake kwa muda wakati wa hafla ya kuzindua mradi wa nyumba za bei nafuu huko starehe ili kuonyesha heshima kwa Adhana.

Adhana ni mwito wa Kiislamu kwa sala ya hadhara katika msikiti unaosomwa na Muadhini katika nyakati zilizowekwa za siku.

Adhana inasomwa kutoka msikitini mara tano kwa siku kwa siku nyingi na kutwa nzima wakati wa likizo za kidini za Idul Fitr na Idul Adha.

Adhana kwa dakika tatu kabla ya Rais kurejelea hotuba yake huku akishangiliwa na kupigiwa makofi makubwa kutoka kwa waliohudhuria kutokana na heshima yake kwa Adhana.

Mnamo Machi 22, 2021, mtangulizi wa Ruto Uhuru Kenyatta aliwagusa waumini wengi wa Kiislamu alipositisha hotuba yake wakati wa Adhana nchini Tanzania alipokuwa akihudhuria misa ya mazishi ya Rais wa zamani John Magufuli.

Uhuru alisimamisha kwa muda hotuba yake kwa muda wa karibu dakika tatu kwa heshima ya Adhana katika msikiti wa karibu mjini Dodoma.

3482731

captcha