IQNA

Waislamu Marekani

Misikiti ya New York wapata idhini ya kuadhini kila Ijumaa

13:48 - August 31, 2023
Habari ID: 3477525
WASHINGTON, DC (IQNA) - Adhana, mwito wa Kiislamu wa Sala, unaweza kutangazwa kwa vipaza Saudi katika Jiji la New York kwa nyakati maalumu kila Ijumaa na wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Meya Eric Adams alitangaza haya katika mkutano wa wanahabari Jumanne, na kuongeza "Kwa muda mrefu sana, kumekuwa na mkanganyiko kuhusu ni jamii zipi haziruhusiwi kutangaza  wito wao wa Sala kwa vipaza sauti."

“Leo tunatangazawazi kwamba misikiti na nyumba za ibada ziko huru kuongeza mwito wao wa kusali Ijumaa na wakati wa Ramadhani bila kibali muhimu,” alisema.

Katika mkutano huo wa wanahabari uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka jumuiya mbalimbali za misikiti na taasisi za Kiislamu, Adams alisema: "Mko huru kutekeleza imani yenu katika jiji la New York kwa sababu, kwa mujibu wa sheria, sote tuna haki ya kutendewa sawa. Utawala wetu unajivunia sana kufikia mafanikio haya."

Chini ya mwongozo mpya, msikiti unaweza kutangaza adhana kila Ijumaa kati ya saa sita na nusu hadi saa saba na nusu mchana na vile vile kabla wa futari kila jioni wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Viongozi kutoka jamii ya Kiislamu walitoa shukrani kwa meya na maafisa wengine. Mkutano ulipomalizika, kuliadhiniwa kwenye jukwaa sambamba na maelezo ya Kiingereza ya maana ya maneno ya Adhana.

3484981

Kishikizo: marekani adhana waislamu
captcha