IQNA

Jinai za Israel

Waumini milioni nne walisali Msikiti wa Al-Aqsa Ramadhani mwaka huu licha ya vizuizi vya Israel

18:53 - April 21, 2023
Habari ID: 3476899
TEHRAN (IQNA)-Idara ya Wakfu wa Kiisalmu katika mji wa Al-Quds (Jerusalem) imetangaza kwamba wamini milioni nne walisali siku mbali mbali katika Msikiti wa Al-Aqsa katika kipindi kizima cha mwezi uliobarikiwa wa Ramadhani licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na utawala haramu wa Israel.

Idara hiyo inayosimamiwa na Jordan ilisema uwepo mkubwa wa Waislamu kwenye eneo hilo takatifu wakati wa Ramadhani ulikuwa wa kushangaza mwaka huu licha ya ukubwa wa vizuizi vya utawala haramu wa Israel kwa lengo la kuwazuia waumini Wapalestina kutoka Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza

Wakati wa Mwezi Mtakatifu, waumini wenye umri wa miaka 12-55 kutoka Ukingo wa Magharibi walizuiwa kuingia katika mji mkongwe wa Quds, ambapo msikiti huo upo, huku idadi ndogo ya mamia  kutoka kwa Ukanda wa Gaza wakiruhusiwa kuingia katika eneo la Msikiti wa Al Aqsa.

Sanjari na likizo ya Wayahudi ya Pasaka mapema Aprili, vikosi vya utawala vamizi wa Israel viliuvamia Msikiti wa Al Aqsa mara mbili na kuwafukuza maelfu ya waumini wa Kiislamu wakiwa katika ibada za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sambamba na kuruhusiwa walowezi wa Kiyahudi wa Israel kuingia eneo hilo takatifu la Kiislamu na hivyo kulivunjia heshima. Uchokozi huo wa Israel ulilaniwa vikali kimataifa.

Tangu 2003, watawala wa Israel wamekuwa wakiruhusu walowezi ndani ya eneo la Msikiti wa Al Aqsa kila siku isipokuwa Ijumaa.

Idara ya Wakfu wa Kiislamu imeelezea kuwa uwepo wa walowezi katika msikiti wa al-Aqsa kuwa ni uchochezi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel uliuteka mji wa Quds Mashariki, ambapo Msikiti wa Al-Aqsa upo, wakati wa vita vya siku sita mnamo 1967 katika harakati ambazo hazijawahi kutambuliwa na jamii ya kimataifa.

3483296

Kishikizo: quds al aqsa
captcha