IQNA

Watetezi wa Palestina

Rais wa Tunisia: Palestina lazima irudi kwa Wapalestina

14:22 - August 31, 2023
Habari ID: 3477527
TUNIS (IQNA) - Rais wa Tunisia amesistiza kuwa nchi yake kati haitaanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel , akisema neno hilo halipo hata katika kamusi ya Tunisia.

Akiwahutubia mabalozi wapya wa Tunisia katika nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu siku ya Jumanne, Rais Kais Saied alisisitiza kwamba Palestina lazima irejee kwa Wapalestina.

Ingawa taifa la Palestina lina mabalozi ... Usisahau haki ya Palestina; haki halali. Suala la Palestina ni suala kuu la taifa zima, na kwa wale wanaozungumzia kuanzisha uhusiano na Israel (tatbee), nasema neno hili halipo kabisa katika kamusi ya Tunisia,” alisema.

Saeid ameongeza kuwa Wapalestina lazima warejeshe haki zao katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu, na kwamba taifa huru la Palestina ambalo mji mkuu wake ni al-Quds (Jerusalem) lazima lianzishwe.

Mapema mwezi huu, Rais wa Vuguvugu la Kitaifa la Ujenzi la Algeria, Abdelkader Bengrina, alionya kwamba Algiers inapaswa "kuchukua tahadhari kuhusu" Tunis.

Haya yanajiri baada ya ziara kadhaa kufanywa nchini Tunisia na maafisa wa Israel ambazo ziliambatana na juhudi za kuanzisha uhusiano

Mapema Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf alidokeza kwamba balozi wa Tunisia nchini Algeria amekanusha vikali hatua yoyote ya kuhalalisha serikali ya Tunisia.

Kwa mujibu wa bunge la Tunisia, Kamati ya Haki na Uhuru tayari ilikuwa imeanza kuangalia kuwasilisha rasimu ya sheria, ikihimiza kuharamishwa uhusiano na utawala haramu wa Israel.

Mnamo Juni 2022, Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia ilikanusha ripoti kuhusu mazungumzo ya kidiplomasia kati ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini na Israel, na kuyataja kuwa ya uwongo.

Chini ya kile kinachoitwa Makubaliano ya Abraham, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan, na Morocco zilitia saini mikataba ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel iliyopitishwa na Marekani pamoja na utawala wa Israel mwishoni mwa mwaka 2020. Wapalestina wameshutumu makubaliano hayo kuwa ni "usaliti" wa malengo yao ya kukomboa ardhi zao zinazokoloniwa na kukaliwa kwa mabavu na Israel.

3484983

Kishikizo: tunisia israel palestina
captcha