IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur’ani nchini Indonesia yavutia wahifadhi 200 wa kike na kiume

21:59 - October 28, 2023
Habari ID: 3477802
JAKARTA (IQNA) - Kituo cha Qur'ani chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) nchini Iraq kimeandaa mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu nchini Indonesia, na ku wahifadhi 200 kutoka kote nchini.

Huu ulikuwa ni mwaka wa sita mfululizo ambapo mashindano ya Qur'ani yalifanyika Jakarta, mji mkuu.

Mkuu wa tawi la idara hiyo mjini Jakarta Dk Abdullah Beik alisema: "Tunasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Mtume wa Rehema kwa muda wa mwezi mzima katika miji tofauti ya Indonesia. Kama sehemu ya maadhimisho haya, tawi letu liliamua kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, chini ya usimamizi wa na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS)."

Aliongeza, “Zaidi ya washiriki 200 wa kike na kiume walishiriki katika shindano hilo, ambalo lilifanyika katika ofisi yetu huko Jakarta.”

 
 

3485770

captcha