IQNA

Walowezi wa Kizayuni walishadidisha hujuma dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa mwaka 2023

18:36 - January 02, 2024
Habari ID: 3478133
IQNA - Idara ya Waqfu ya Kiislamu huko al-Quds (Jerusalem) imesema kumeshuhudiwa ongezeko la idadi ya walowezi wa Kizayuni waliouhujumu Msikiti wa Al-Aqsa mwaka jana.

Mnamo mwaka wa 2023, walowezi wa Kizayuni wasiopungua 48,000 walivamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa huko katika mji wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel, kwa mujibu wa mamlaka inayosimamia eneo hilo takatifu.

Afisa katika Idara ya Wakfu ya Kiislamu mjini al Quds amesema katika mwaka uliopita, "walowezi 48,223 walivamia jengo la Msikiti wa Al-Aqsa."

Mwezi uliopita pekee, alisema, walowezi 3,086 walivamia msikiti huo chini ya ulinzi wa polisi wa utawala ghasibu wa Israel.

Polisi wa Israel walianza kuwaruhusu walowezi kuingia katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa mwaka 2003, licha ya kulaaniwa vikali na Wapalestina.

Msikiti wa Al-Aqsa ni eneo la tatu kwa utakatifu duniani kwa Waislamu.

Aidha Kituo cha Habari cha Wadi Hilweh chenye makao yake mjini al Quds kimesema katika taarifa yake kwamba mamlaka za Israel zilitoa amri 1,105 za kuwatimua Wapalestina mwaka 2023, zikiwemo za kuwatimua kutoka Mji Mkongwe wa al-Quds na kwingineko katika jiji hilo.

Kituo hicho pia kilinakili ubomoaji 209 wa Israel wa nyumba za Wapalestina katika eneo la Al Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na ubomoaji 68 ambao ulifanyika baada ya Oktoba 7, kuanza kwa mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Israel iliikalia kwa mabavu Al-Quds Mashariki, ambako Al-Aqsa iko, wakati wa Vita vya Waarabu na Israel vya mwaka 1967 (Vita vya Siku Sita). Ilitwaa jiji lote mwaka wa 1980, katika hatua ambayo haijatambuliwa kamwe na jumuiya ya kimataifa.

3486647

Habari zinazohusiana
captcha