IQNA

Kipindi cha Televisheni cha Mahfel katika picha

IQNA- Kipindi cha Televisheni cha Mahfel Msimu wa Pili kilianza kuonyeshwa Machi 12 sambamba na kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kanali ya 3 ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB)

Hutangazwa kabla ya Magharibi  kila siku katika mwezi mtukufu, na kutoa mahali pazuri pa kiroho kwa watazamaji wanapojitayarisha kufuturu.

Kipindi hicho ambacho kimelenga zaidi kuangazia ujuzi wa Qur'ani kinatoa fursa kwa watu walio katika saumu kusikiliza mijadala yenye mafundisho pamoja na usomaji wa Qur'ani wenye mvuto.

Kipengele muhimu kinachochangia mvuto wa programu hiyo ni kujumuishwa kwa wataalamu wa Qur'ani, hasa wasomi mashuhuri wa kigeni kama vile Sayyid Hassanayn al-Hulw kutoka Iraq na Rizwan Darwish kutoka Syria. Programu hiyo pia ina wataalam wawili wa Iran, ambao ni maqari mashuhuri Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi.