IQNA

Pakistan yaitaka India ilinde haki za Waislamu

17:35 - December 07, 2020
Habari ID: 3473432
TEHRAN (IQNA) – Pakistan imetoa wito kwa serikali ya India ilinde haki za jamii za waliowachache hasa Waislamu na ihakikishe kuwa wanapata usalama na uhuru wa kuabudu.

 Katika taarifa Jumatatu, Wizara ya Mambo ya India imekumbusha tukio la Disemba 6 miaka 28 iliyopita wakati Wahidi wenye misimamo mikali waliuvamia msikiti wa kihistoria wa Babri nchini India. Taarifa hiyo imesema msikiti huo uliojengwa karne kadhaa huko Ayodhya na ulivunjwa na Wahindi wenye misimamo ya kufurutu ada wanaofuta itikadi za wanamgambo wa mrengo wa kulia wa RSS ambao ni wafausi wa chama tawala cha sasa cha India cha BJP.

Pakistan pia imetoa wito kwa jamii ya kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, kuchukua hatua za kulinda turathi za Kiislamu nchini India ambazo zinakabiliwa na hatari ya kuvunjwa na utawala wa nchi hiyo wenye utaifa wa Kihindu maarufu kama Hindutva.

Tarehe 6 Disemba miaka 28 iliyopita, Wahindu wenye misimamo mikali waliubomoa Msikiti wa Babri katika mji wa Faizabad kwenye jimbo la Uttar Pradesh nchini India. Msikiti huo ulijengwa mwaka 1528 na Zahiruddin Muhammad Babur juu ya kilima na tangu wakati huo ulijulikana kwa jina la Msikiti wa Babri. Baada ya kupita karne tatu tangu ujengwe yaani mwaka 1855, mtawala mmoja Muingereza alipotosha ukweli kwa makusudi na kuandika kuwa msikiti huo umejengwa kwenye magofu ya jumba la ibada ya masanamu la Wahindu. Suala hilo lilikuwa chanzo cha fitina na ugomvi mkubwa kati ya Waislamu na Wahindu. Mwaka 1992 Wahindu wenye misimamo ya kufurutu mipaka walivamia Msikiti wa Babri na kuubomoa kikamilifu, suala ambalo lilizusha vita baina ya Waislamu na Wahindu au kwa jina jingine Mabaniani.

3939519

captcha